Swahili Rock Climbing Glossary of Terms
Ambatanisha Kuweka mikono yote au miguu yote kwa kishikio sawa. Taz. leta pamoja. Match
Bilei Mbinu inayotumika kushikilia kamba ili kuzuia kuanguka kwa mpandaji. Inashirikisha kuchukua kamba kutoka mpandaji kwa kupitia kifaa cha bilei au kupatia mpandaji kamba kupitia kifaa cha belei. Belay
Bita Maarifa au habari jinsi ya kukamilisha njia au tatizo unalopanda kwa mwamba. Namna hatua zinavyopaswa kuwa na jinsi unavyopaswa kuzifanya. Kawaida huambiwa na mtu ambaye amekamilisha njia au tatizo hilo hapo awali. Taz. mwakenya. Beta
Chaki Kitu namna ya udongo mwororo aghalabu cheupe kinachotumiwa kwa mikono na mpandaji ili kuiweka mikono kavu na kuboresha akamatavyo vishikio. Chalk
Cheki Kusaidia kuelekeza mpandaji wakati wa kuanguka haswa anapokwea tatizo ama anapoanza kuongoza njia. Nicheki. Spot
Chukua! Neno linalotumiwa na mpandaji kuonya mdhibiti kwamba ulegevu wa kamba unahitaji kupunguzwa. Take!
Enda upande Kuchukua hatua kwa upande kwenye sehemu ya mwamba wakati wa kupanda. Traverse
Finya 1. Kishikio ambacho kinabanwa kati ya kidole cha gumba na vidole vingine. 2.Kubana kishikio kati ya kidole cha gumba na vidole vingine. Pinch
Cheki/spot
Fuata Kupanda nyuma au baada ya kiongozi ukiondoa na kukusanya gia ambazo ameweka njiani. Follow
Fukiza Kutoa bita pana kwa mpandaji, mara nyingi isiyohitajika ama isiyouliziwa. Spray
Gea Taz. gia. Gear
Gia Vifaa anavyotumia mpandaji kupunguza ajali anapopanda; huwezesha kupanda kwa ustadi. Taz. gea. Gear
Godoro Tandiko nene ambalo linalotumika kama kinga ya kuanguka kwa mpandaji anapopanda bila kamba. Linatengenezwa na sponji na linaweza kubebwa. Crash Pad
Hanesi Vazi linalovaliwa kwenye nyonga na kwenye mapaja. Lina nafasi mbili zinazotenganishwa za kupenyezea miguu. Huvaliwa kwenye upandaji wowote wa kamba kwani ni vazi muhimu kwa usalama. Harness
Helmeti Kofia ya sandarusi ya kukinga kichwa kisidhuriwe na pigo kutoka kwa mwamba au uchafu unaoanguka; huvaliwa wakati wa kupanda. Helmet
Jabali Mwamba mkubwa. Kilima au mlima wa mwamba. Taz. mawe. Crag
Jongea Matembezi yanayohitajika kufikia kwenye msingi wa mwamba au jabali. Taz. Karibia. Approach
Kamba Uzi mnene uliotengenezwa kwa kusokota nyusi nyembaba pamoja. Hutumika kwenye aina tofauti za kupanda. Yaweza kuwa tuli au yenye nguvu. Rope
Kamba inajivuta Msuguano unaosababishwa wakati kamba ya kupanda inapita juu ya mawe au kwa gia haswa kwa namna isiyo kiwimawima. Rope drag
Kamilisha Kupanda njia au tatizo bila kuanguka kwenye jaribio la kwanza, na bila mwakenya au bita ya kupanda. Flash
Karabina Kitanzi cha chuma kilicho na lango upande mmoja. Hutumiwa kwa mifumo ya usalama inayotumika wakati wa kupanda. Carabiner
Karibia Taz. jongea. Approach
Jongea/Approach
Kausha Mpandaji anapoukaza mwili wako katika nafasi moja huku akishikilia kishikio kwa mkono mmoja uliokunjwa na uzito mwingi ukiwa kwenye bega; kawaida wakati mpandaji anapofikia kishikio kingine. Lock-off
Kifaa cha bilei Kifaa maalum ambacho hutumiwa kusaidia mdhibiti kudhibiti kamba ya mpandaji. Kikitumiwa kwa usahihi, kifaa cha bilei huunda msuguano wa kamba ambao humsaidia mdhibiti kushika mpandaji akianguka, kumshukisha au kumlegezea kamba anapoongoza njia. Belay Device
Kiongozi Mpandaji anayetangulia kwenye njia mbele ya wengine ili kuelekeza njia kwa wenzake huku akiweka gia mara kwa mara kama kinga na kubandika kamba ndani ya gia. Leader
Kishikio Umbo ambao kwa kawaida huambatanishwa na ukuta wa kupanda ili wapandaji waweze kuushika au kuukanyaga. Hold
Kupanda bila kamba Aina ya kupanda tatizo kwenye mwamba. Kwa kawaida, godoro huwekwa chini ya tatizo kama mahali pazuri pa kutua ili kupunguza ikiwa mpandaji ataanguka au kuruka chini kutoka juu ya tatizo. Bouldering
Kupanda kwanza Kitendo cha kuwa mtu wa kwanza kupanda njia au tatizo kwa mtindo fulani. First Ascent
Kupanda kwa kamba Kuelekea juu ya jabali ukiwa umefungwa kwenye kamba inayodhibitiwa na mtu mwingine (mdhibiti). Kuna aina tofauti vya kupanda kwa kamba. Roped climbing
Legeza! Neno linalosemwa na mpandaji kumweleza mdhibiti aongeze ulegevu kwa kamba anapopanda. Slack!
Leta pamoja Taz. Ambatanisha. Match
Kishikio/climbing hold
Mawe/ Rock
Mawe Hutumika mara kwa mara kumaanisha eneo la kupanda; jabali ama mwamba. Rock
Mdhibiti Mtu anayeshughulikia kamba kupitia kifaa cha bilei ili kumshika mpandaji ikiwa ataanguka au kuteleza anapopanda. Belayer
Mfuko Kishikio ambacho ni shimo au pango la duara kwenye mwamba ambacho unaweza kuingiza kati ya kidole kimoja au vidole vinne lakini sio mkono mzima. Pocket
Mfuko wa chaki Kifuko kidogo cha kushikilia chaki. Kawaida hufungwa kwa kamba na kuvaliwa kiunoni. Chalk bag
Mpandaji Mtu anayejihusisha na shughuli ya kupanda jabali au miamba. Climber
Mtelezo Kishikio cha mviringo laini ambacho kinahitaji kushikwa na kiganja chote kwa sababu ya asili yake ya kuteleza. Sloper
Mwakenya Taz. bita. Beta
Mwamba Jiwe kubwa lilio chini kama kwamba mpandaji anaweza kuanguka kwa usalama majini au kwa godoro lililo kwenye nchi kavu. Boulder
Mwanzilishi Mpandaji aliye wa kwanza kupanda njia au shinda maalum kwa mtindo fulani. First Ascender
Nanga Kifaa au mfumo wa kufunga kamba au kupachika mpandaji juu ya sehemu ya kukwea ili kuwezesha mpandaji kukamatwa anapoanguka na kuzuia mpandaji kuanguka. Anchor
Njia Sehemu maalum inayofaa kupitiwa ili kukamilisha ukweaji kwa jabali. Route
Mwamba/ boulder
Noma Sehemu ngumu zaidi ya kupanda au mwendo mgumu zaidi katika kupanda. Mahali ambapo mpandaji anaweza kuanguka kwa urahisi. Crux
Ongoza Mtindo wa kupanda ambapo mpandaji anatangulia kwenye njia huku akiweka gia mara kwa mara kama kinga na kubandika kamba ndani ya gia. Lead
Rukia Namna ya kupanda ambayo mpandaji anaruka au kusonga kwa nguvu kutoka kwa kishikio kimoja hadi kufika mbali kwenye vishikio vingine. Dyno
Safisha Kuchukua vipande vyote vya gia ambavyo vilitumika kwa kupanda, baada ya kumaliza kupanda. Inahusu pia kuandaa mwamba kwa kuondoa uchafu kwa njia au tatizo mpya. Clean
Shuka Enda chini kutoka juu. Kufanya ukoo unaoudhibiti mwenyewe kwenye kamba; teremka. Abseil/rappel
Shukisha Letwa chini kutoka juu. Kufanya ukoo unaodhibitiwa kwenye kamba na mdhibiti; teremsha. Lower
Shushu Kipande kikubwa cha ngozi ambacho huegemea kidoleni baada ya kuvutwa kwenye mawe. Flapper
Tatizo Sehemu maalum inayofaa kupitiwa ili kukamilisha ukweaji kwa mwamba ambapo mpandaji hatumii kamba. Pia Changamoto. Problem
Tetemeka Tikisika kwa harakaharaka bila kudhibiti kwa mguu mmoja wakati mpandaji ana wasiwasi, anaogopa, au amechoka kwenye mwamba. Shaking/Elvis Legs
Thabiti Kipande cha gia au nanga ambacho kinadhaniwa kuwa imara. Bomber
Tokea juu Hatua ya mwisho juu ya tatizo ambayo inajumuisha mpandaji kutokea juu ya mwamba. Top-out
Tuma Kupanda njia au tatizo kutoka chini hadi juu bila kuanguka au kupumzika kwa gia. Send
Twanga Kutuma njia au tatizo kwa mtindo mzuri, au kujaribu kwa bidii wakati wa kutuma. Crush
Shukisha/ Lower
Twende! Neno linalotumika kutia mpandaji moyo wakati anapopanda kwa bidii kwenye njia au tatizo, haswa kwenye sehemu noma. Come on! Allez!
Ufa Mpasuko au mgawanyiko ulioko kwenye mwamba na ambao unaruhusu uwekaji wa gia wakati wa kupanda na ambao hutumiwa kwa mikono na miguu wakati wa kupanda. Crack
Ulegevu Kamba ya ziada kati ya mdhibiti na mpandaji. Slack
Viatu vya kupanda Viatu vilivyoundwa mahsusi kulinda miguu na kutoa msuguano unaohitajika mpandaji anapokwea kwenye mawe. Climbing Shoes
Vishikio Wingi wa kishikio. Climbing hold
Vuta upande 1. Aina ya kishikio ambacho kinaruhusu mpandaji kupanda akivuta kutoka upande. 2. Jinsi ya kukamata ambayo inajumuisha kuvuta kwa mkono na kusukuma kwa miguu. Side-pull
Waka Mikono inapobana na kufanya mpandaji kutoweza kuushika vishikio vizuri. Hali hii hupatikana wakati mpandaji anapopanda kwa muda mrefu au kutokana na kuufanya mwendo unaostahili nguvu nyingi. Pumped
Wa pili Mpandaji anayefuata kiongozi kwenye jabali. Second
Viatu via kupanda/climbing shoes
Want to contribute to the list? Write to us here.